SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 26, 2011

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA KIMATAIFA WA MAWASILIANO ICT!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT) uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana.
Mawaziri wakipiga makofi kumpongeza Makamu wa Rais baada ya kumaliza hotuba yake.
Waziri wa Elimu wa na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa akizungumza baada ya makamu wa rais kufungua mkutano huo.
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu wao waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo wakifuatilia maonyesho ya picha zilizokuwa zikionyeshwa katika Screen za ukutani.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Samwel Muro wakati alipotembelea banda lao la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils)  wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa  sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi Elimu na Mafunzo (ICT) uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni  Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj.
Prof .Tibaijuka naye akijaribu miwani hiyo ili kuona picha hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Imelda Lutebinga na Langton Chibura wakati alipotembelea Banda lao la maonyesho la SEACOM Tanzania Ltd baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT) uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipongezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana.
Makamu wa Rais katika picha ya pamoja na baadhi ya watu walio present paper zao.
(Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment